KARIAKOO DERBY, Kocha wa Yanga Hamdi Atoa Kauli ya Kujiamini

KARIAKOO DERBY, Kocha wa Yanga Hamdi Atoa Kauli ya Kujiamini | Kocha wa Yanga SC Hamdi Miloud ameonyesha kujiamini kuelekea mchezo wa watani wa jadi Simba SC huku akisisitiza kuwa hawana wasiwasi kwa sababu wao ni timu kubwa.

KARIAKOO DERBY, Kocha wa Yanga Hamdi Atoa Kauli ya Kujiamini

“Sisi ni timu kubwa, sisi ni Young Africans, kwa nini tuwe na wasiwasi?” alisema Miloud akionyesha imani kubwa kwa kikosi chake kabla ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Hata hivyo kocha huyo amekiri kuwa kuna wasiwasi juu ya hali ya nyota wake Stephane Aziz Ki ambaye anasumbuliwa na nyonga na hatima yake ya kuwa mchezaji bado haijafahamika.

KARIAKOO DERBY, Kocha wa Yanga Hamdi Atoa Kauli ya Kujiamini

Wakati huohuo nahodha msaidizi wa Yanga Dickson Job amesema wao wakiwa wachezaji wamejipanga kupambana kuhakikisha wanapata pointi tatu kwenye mchezo wa Kariakoo Derby.

Mechi hii inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini, huku pande zote mbili zikiwa na hamu ya kulitawala jiji la Dar es Salaam.

Kocha anasema nimchezaji mmoja tu ambaye ataukosa mchezo huwo nae ni Aziz Ki ambapo anamaumivu kwenye nyongo, hivyo asilimia ni 50% kucheza na kutokucheza. Hili ni pengo kubwa sana kwa Yanga kwakuwa Azizi amechangia magoli mengi zaidi kwenye michezo ya dabi.

ANGALIA PIA: