Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo 2025 | Kocha Hemedi Moroco aitaja Taifa Stars kwa ajili ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Hemedi Moroco ametangaza rasmi kikosi cha Taifa Stars kitakachoshiriki mechi mbili muhimu za kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Congo na Morocco mwezi Machi.
Mabadiliko madogo kwenye kikosi
Hakuna mabadiliko makubwa kwenye kikosi hiki kutoka kwenye kikosi kilichopita, jambo ambalo linaonyesha kuwa timu ya makocha ina imani kubwa na wachezaji waliopo.
Timu hii inatarajiwa kupambana vilivyo kuhakikisha Taifa Stars inapata angalau pointi 4 katika michezo hii miwili, ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa mara ya kwanza katika historia ya soka la Tanzania.
Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Leo 2025
Wachezaji Walioitwa:
- Yakoub Suleiman (JKT Tanzania)
- Ally Salim (Simba SC)
- Hussein Masaranga (Singida BS)
- Shomari Kapombe (Simba SC)
- Lusajo Mwaikenda (Azam FC)
- Mohamed Hussein (Simba SC)
- Pascal Msindo (Azam FC)
- Mirajy Abdallah (Coastal Union)
- Ibrahim Abdulla (Young Africans)
- Dickson Job (Young Africans)
- Abdulrazack Mohamed (Simba SC)
- Ibrahim Ame (Mashujaa FC)
- Haji Mnoga (Salford City, Uingereza)
- Novatus Miroshi (GΓΆztepe FC, Uturuki)
- Mudathir Yahya (Young Africans)
- Yusuph Kagoma (Simba SC)
- Feisal Salum (Azam FC)
- Charles M’Mombwa (Newcastle United Jets, Australia)
- Kibu Denis (Simba SC)
- Simon Msuva (Al-Talaba SC, Iraq)
- Clement Mzize (Young Africans)
- Iddy Selemani (Azam FC)
- Selemani Mwalimu (Wydad Casablanca, Morocco)
- Kelvin John (Aalborg BK, Denmark)

Ratiba ya Michezo ya Taifa Stars β Machi 2025
π
17 Machi 2025 – πΉπΏ Tanzania vs Congo
π
26 Machi 2025 – π²π¦ Morocco vs Tanzania
Mashabiki wa soka nchini watakuwa na matumaini ya kuiona Stars ikicheza kwa nidhamu na kujitahidi kupata matokeo mazuri katika mechi hizo muhimu. Ushindi dhidi ya Congo nyumbani na sare angalau dhidi ya Morocco ugenini utaongeza matumaini ya Taifa Stars kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako