Mashabiki wa Yanga Wajitokeza Nje ya Uwanja wa Mkapa Wakati wa Kikao cha Kujadili Hatma ya Kariakoo Dabi | Baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga SC wamejitokeza nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo kunafanyika kikao muhimu kati ya viongozi wa TFF, Serikali, Bodi ya Ligi, Simba SC, na Yanga SC.
Mkutano huu unalenga kutafuta suluhu kuhusiana na mechi ya Kariakoo Dabi, iliyokuwa ichezwe Machi 8, 2025, lakini ikaahirishwa.
Hadi sasa bado hakuna taarifa rasmi kuhusu maamuzi yanayoweza kuibuka kwenye mkutano huo, lakini uwepo wa mashabiki wa Yanga nje ya uwanja unaonyesha ukubwa wa umuhimu wa mechi hii kwa wadau wa soka nchini.

Macho na masikio ya mashabiki wa soka yameelekezwa kwenye kikao hiki, ambapo hatima ya mchezo huu mkubwa inatarajiwa kuamuliwa. Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi kuhusu maamuzi yatakayofanywa.
Mashabiki wa Yanga Wajitokeza Nje ya Uwanja wa Mkapa Wakati wa Kikao
#MICHEZO Baadhi ya Mashabiki na Wanachama wa klabu ya Yanga wamejitokeza nje ya uwanja wa Benjamini Mkapa ambako kinafanyika kikao cha viongozi wa TFF, Serikali na viongozi wa vilabu vya Simba na Yanga. Kikao ambacho kinafanyika kutafuta suluhu ya mchezo wa Kariakoo dabi ambao… pic.twitter.com/M9i2ji0vny
— EastAfricaTV (@eastafricatv) March 27, 2025
CHECK ALSO:
Weka maoni yako