Matokeo ya Azam vs Tanzania Prisons Leo 06/03/2025 | Azam FC vs Tanzania Prisons: Mechi Muhimu ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mchezo kati ya Azam FC na Tanzania Prisons utachezwa Machi 6, 2025 kuanzia saa 18:00 UTC. Mchezo huu ni sehemu ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi za timu hizo kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Matokeo ya Azam vs Tanzania Prisons Leo 06/03/2025

Msimamo wa Timu Kabla ya Mechi
- Azam FC: Nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.
- Tanzania Prisons: Nafasi ya 14, ikipambana kuepuka kushuka daraja.
- Rekodi ya Hivi Karibuni: Timu hizi zilishakutana mara moja msimu huu, na mchezo hu0 Azam aliibuka na ushindi wa goli 2-0 uwanja wa Sokoine Mbeya.
Umuhimu wa Mechi kwa Timu Zote
- Azam FC inahitaji ushindi na alama zote 3 ili kuendelea kusalia kwenye mbio za ubingwa wa ligi msimu huu. Kupoteza alama katika mechi hii kunaweza kuwa pigo kubwa kwa matumaini yao ya kutwaa taji.
- Tanzania Prisons wanalenga kupata matokeo mazuri ili kujiweka salama na kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja. Alama 3 zitakuwa muhimu sana kwao katika jitihada za kuboresha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali, huku kila timu ikihitaji ushindi kwa sababu tofauti. Azam FC itashuka uwanjani ikiwa na lengo la kujiweka sawa katika mbio za ubingwa, huku Tanzania Prisons ikihitaji ushindi ili kuepuka kushuka daraja.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako