Matokeo ya Leo NBC Primier League 07 Machi 2025 | Kagera Sugar yashinda huku JKT Tanzania ikielekea ushindi.
Kagera Sugar wamepata ushindi wa nne katika msimu huu wa ligi kuu ya NBC 2024/2025 baada ya kuifunga Pamba ya Jiji kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa leo Machi 7, 2025. Ushindi huu ni wa kwanza kwa kocha mpya wa timu hiyo Juma Kaseja ambaye ameanza vyema kazi yake ya ukocha mkuu.
Katika mechi nyingine, JKT Tanzania ilipata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Tabora United. Hii ni mara ya kwanza kwa Tabora United kupoteza mechi tangu ilipofungwa na Simba SC Februari 2, 2025.
Matokeo ya Leo NBC Primier League 07 Machi 2025
Kagera Sugar 2-1 Pamba Jiji
- Kagera Sugar yashinda kwa mara ya nne msimu huu.
- Kocha Juma Kaseja aandika historia kwa kupata ushindi wake wa kwanza kama kocha mkuu.

Tabora United 1-2 JKT Tanzania
- Tabora United yapoteza kwa mara ya kwanza baada ya michezo sita mfululizo bila kushindwa.
- JKT Tanzania yaendeleza rekodi nzuri kwenye ligi.
Msimamo wa ligi unazidi kuwa mgumu huku timu zikihitaji pointi muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri kuelekea mwisho wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC wa 2024/2025. Mashabiki wa soka wakiendelea kushuhudia mchuano mkali huku Simba SC na Yanga SC zikijiandaa na mchezo wa Kariakoo derby unaotarajiwa kufanyika kesho.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako