Mbappe Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Real Madrid

Mbappe Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Real Madrid, Je, Ndiye Mrithi Rasmi? | Kylian Mbappé aliendelea kuthibitisha thamani yake akiwa Real Madrid baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Leganés kwenye Uwanja wa Santiago Bernabéu.

Mbappe Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Real Madrid

Akiwa na mabao hayo, Mbappé sasa ana mabao 33 katika msimu wake wa kwanza akiwa na Real Madrid, sawa na Cristiano Ronaldo aliofunga mara ya kwanza akiwa na Real Madrid msimu wa 2009/10.

Mabao yake mawili dhidi ya Leganés yalikuwa ya kipekee, moja la penalti na lingine la faulo dakika ya 76, na kuhakikisha Madrid inasalia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania taji la La Liga msimu huu.

Licha ya kuwiana na Ronaldo, kuna tofauti moja kuu: Ronaldo alihitaji mechi 35 pekee kufikia hatua hii muhimu, wakati Mbappé ameichezea Real Madrid mara 45 msimu huu. Hata hivyo, hii haipunguzii mafanikio ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa, ambaye ameonyesha uwezo mkubwa tangu atue kwa wababe hao wa Uhispania.

Mbappe Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Real Madrid
Mbappe Aifikia Rekodi ya Cristiano Ronaldo Real Madrid

Kwa mafanikio haya, swali linabaki: Je, Kylian Mbappé ndiye mrithi wa kweli wa Cristiano Ronaldo pale Real Madrid? Wengi wanaamini kuwa anaweza kufuata nyayo za nyota huyo wa Ureno, lakini bado ana mengi ya kuthibitisha kabla ya kufikia hadhi ya mchezaji wa kihistoria.

CHECK ALSO: