Mbeya City Yaitupa Azam Nje CRDB Bank Federation Cup 2024/2025 | Mbeya City Yaitoa Azam FC Kwa Penalti na Kusonga Hatua ya 16 Bora Federation Cup.
Timu ya Mbeya City imefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora ya michuano ya CRDB Bank Federation Cup 2024/2025 baada ya kuiondosha Azam FC kwa mikwaju ya penalti, kufuatia sare ya 1-1 katika muda wa kawaida wa mchezo.
Mbeya City Yaitupa Azam Nje CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
Matokeo ya Mchezo
⏱ Full Time:
Azam FC 1️⃣-1️⃣ Mbeya City

Mikwaju ya Penalti:
- Azam FC: ✅✅❌❌
- Mbeya City: ✅❌✅✅✅
Kwa ushindi huo, Mbeya City imekata tiketi ya hatua inayofuata na kusababisha Azam FC kuaga mashindano katika hatua ya awali.
Baada ya kupata matokeo ya sare ndani ya dakika 90, Azam walikosa penalti mbili muhimu ambazo ziliwapa Mbeya City nafasi ya kusonga mbele.
Mbeya City sasa inajiandaa kwa mechi ya 16 Bora katika harakati za kutafuta taji la CRDB Bank Federation Cup 2024/2025.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako