Mechi ya Kariakoo Derby Yaahirishwa Rasmi na TPLB | Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeahirisha rasmi mchezo wa watani wa jadi Yanga SC dhidi ya Simba SC uliokuwa uchezwe leo Jumamosi Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mechi ya Kariakoo Derby Yaahirishwa Rasmi na TPLB
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya TPLB, uamuzi wa kuahirisha mchezo huo ulitolewa baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kupitia malalamiko ya Simba SC, iliyodai kuzuiwa kuingia uwanjani kwa ajili ya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo.
Sababu za kuahirishwa kwa mechi
Taarifa ya TPLB inaeleza kuwa ofisa huyo wa usalama wa mchezo aliwasilisha taarifa rasmi ya tukio la kutofanya mazoezi kwa Simba SC pamoja na matukio mengine yanayohitaji uchunguzi zaidi.

Bodi ya Ligi imebainisha kuwa:
- Baadhi ya matukio yanahitaji uchunguzi wa kina, ambao hauwezi kukamilika kwa muda mfupi.
- Uamuzi wa kuahirisha mechi umetolewa ili kuhakikisha haki inatendeka na kuhakikisha mazingira bora ya mchezo.
Kwa sasa, TPLB haijatangaza tarehe mpya ya mchezo huo lakini imeahidi kutoa taarifa zaidi mara itakapokamilisha uchunguzi wake.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania walikuwa na shauku ya kushuhudia mchezo wa Kariakoo derby lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza, mechi hiyo itachezwa tarehe nyingine itakayotangazwa rasmi na mamlaka husika.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako