Picha za Uwanja wa Airtel Stadium Singida Black Stars | Singida Black Stars kufungua uwanja mpya, AIRTEL STADIUM, Machi 24: Somo kwa Simba na Yanga?
Picha za Uwanja wa Airtel Stadium Singida Black Stars
VIDEO: Uwanja wa Airtel Stadium unaomilikiwa na Singida Black Stars 🇹🇿 pic.twitter.com/X5zPGAJN4b
— FELIX JASON (@Iamfelixtz) March 24, 2025
Klabu ya Singida Black Stars imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya soka kwa kutangaza kufungua uwanja wake mpya wa AIRTEL STADIUM Machi 24, 2025. Uwanja huo utazinduliwa kwa mechi ya kirafiki kati ya Singida Black Stars na mabingwa watetezi Yanga SC.
Katika taarifa rasmi ya klabu, Singida Black Stars imethibitisha kuwa uwanja huo umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa uwanja mkubwa wa mashindano ya kitaifa na kimataifa. Hii ni hatua kubwa kwa klabu hiyo inayoendelea kuwekeza kwenye miundombinu yake ili kukuza soka la Tanzania.

Je, hili ni somo kwa Simba na Yanga?
Kwa muda mrefu klabu kubwa za Tanzania, Simba SC na Yanga SC, zimekuwa zikitegemea viwanja vinavyomilikiwa na serikali mfano Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi zao za nyumbani. Pamoja na mafanikio yao makubwa kitaifa na kimataifa, bado hawajaanzisha viwanja vyao.
Uwekezaji wa Singida Black Stars katika Uwanja wa Airtel unaweza kuwa fundisho kwa klabu kubwa kama Simba na Yanga kuelewa umuhimu wa kuwa na viwanja vyao. Kuwepo kwa uwanja wa kisasa kunaipa klabu uhuru wa kupanga ratiba ya mechi, kuongeza mapato yake kupitia matukio mbalimbali, kuboresha mazingira ya mazoezi na maandalizi ya timu.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako