Rasmi Simba SC vs Stellenbosch FC Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF 2024/25

Rasmi Simba SC vs Stellenbosch FC Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF 2024/25: Simba SC Kukutana na Stellenbosch FC Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF.

Rasmi Simba SC vs Stellenbosch FC Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF 2024/25

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imefuzu rasmi hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024 baada ya kuitoa Al Masry ya Misri kwa mikwaju ya penalti 4-1. Mchezo wa robo fainali ya pili ulimalizika kwa sare ya 2-2, na mshindi kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Rasmi Simba SC vs Stellenbosch FC Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF 2024/25
Rasmi Simba SC vs Stellenbosch FC Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF 2024/25

Kwa ushindi huo wa kishujaa, Simba SC sasa itamenyana na Stellenbosch FC ya Afrika Kusini katika hatua ya nusu fainali. Stellenbosch iliwaondoa mabingwa wa zamani wa Afrika Zamalek SC kwa jumla ya 1-0. Hii ni safari ya kipekee kwa timu zote zinazosaka nafasi ya kutinga fainali ya Kombe hili la pili kwa ukubwa la Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Kwa mujibu wa ratiba rasmi iliyotolewa na CAF, Simba SC itacheza mechi ya nusu fainali ya kwanza nyumbani Dar es Salaam, kabla ya kwenda Afrika Kusini kwa mkondo wa pili. Hii ni fursa ya kihistoria kwa klabu ya Tanzania kutinga fainali ya michuano hiyo muhimu barani Afrika.

Rasmi Simba SC vs Stellenbosch FC Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF 2024/25
Rasmi Simba SC vs Stellenbosch FC Nusu Fainali Kombe la Shirikisho CAF 2024/25

RATIBA YA SIMBA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO 2024/25

Simba SC vs Stetellenbosch FC – Aprili 20, 2025

Stellenbosch FC vs Simba SC – Aprili 27, 2025

Mashabiki wa Simba SC wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao kwenye mechi za nyumbani, huku wakiheshimu taratibu za usalama na maadili ya kimichezo. Mashabiki wanaosafiri nje ya nchi pia wanakumbushwa kuheshimu sheria za nchi zao.

Simba SC ina nafasi kubwa ya kuweka historia katika soka la Afrika mwaka huu. Mechi dhidi ya Stellenbosch FC inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, na maandalizi ya kina yatahitajika ili kufikia ndoto ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF.

CHECK ALSO: