Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025 | Msimu wa 2024-2025 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, maarufu kwa jina la Ligi Kuu ya NBC 2024/2025, unatarajiwa kuanza kwa kishindo Agosti 16, 2024. Msimu huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua zaidi huku timu 16 zikiwa zimechuana vikali kuwania ubingwa.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) imetangaza rasmi kuanza kwa msimu mpya wa 2024-25 wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 16, 2024.
Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025, Msimu huu unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na maboresho yaliyofanywa kwenye vikosi vya timu kadhaa ambazo zote zimeonyesha wazi nia ya kutaka kuipa changamoto Yanga Sc kutetea ubingwa wao.
Kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu, mashabiki wa soka watashuhudia mechi ya Ngao ya Jamii, itakayochezwa kati ya tarehe 8 na 11 Agosti 2024. Mechi hii ya jadi itakuwa kipimo cha awali cha uwezo wa timu kabla ya kuanza kwa msimu rasmi/Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025.
Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025
Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inaelekea ukingoni huku raundi ya 29 ikitarajiwa kuchezwa Jumatano hii, tarehe 18 Juni 2025. Katika hatua hii muhimu ya msimu, jumla ya mechi nane zitachezwa kwa wakati mmoja, saa 10:00 jioni
Mashujaa vs JKT Tanzania β Sinema Zetu
Pamba Jiji vs KMC FC β UTV
Simba SC vs Kagera Sugar β Azam Sports 2 HD
Namungo vs KenGold β Azam TWO
Singida BS vs Tanzania Prisons β Azam Sports 4 HD
Young Africans vs Dodoma Jiji β Azam Sports 1 HD
Coastal Union vs Tabora United β Azam ONE
Fountain Gate vs Azam FC β Azam Sports 3 HD

Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa msimu wa 2023-2024 watakuwa na kibarua cha kutetea ubingwa wao dhidi ya timu nyingine kali. Msimu huu, Ligi Kuu itawakaribisha wapya Kengold FC kutoka Tukuyu, Mbeya, na Pamba Jiji FC ya Mwanza, ambazo zote zimepanda daraja kutoka Daraja la Kwanza/Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako