Rekodi za Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania

Rekodi za Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania | Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania imekuwa na ushindani mkubwa tangu kuanzishwa kwake, huku klabu kadhaa zikionyesha ubora wao kwa nyakati tofauti. Hadi sasa Simba Queens ndio wanaongoza kwa kutwaa ubingwa mara nyingi zaidi (mara 4), ikifuatiwa na JKT Queens (mara 3) na Mlandizi Queens (mara 1).

Rekodi za Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania

Orodha ya Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania

  • 2017 – Mlandizi Queens 🏆
  • 2017/2018 – JKT Queens 🏆
  • 2018/2019 – JKT Queens 🏆
  • 2019/2020 – Simba Queens 🏆
  • 2020/2021 – Simba Queens 🏆
  • 2021/2022 – Simba Queens 🏆
  • 2022/2023 – JKT Queens 🏆
  • 2023/2024 – Simba Queens 🏆
  • 2024/2025 – ❓ (Nani atatwaa ubingwa msimu huu?)

Msimu huu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku timu kadhaa zikionyesha uwezo wa kuwania ubingwa. Simba Queens ambao wametwaa ubingwa mara nne, wanaingia msimu huu wakiwa mabingwa watetezi na moja ya timu zenye nafasi kubwa ya kutwaa tena taji hilo.

Rekodi za Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania
Rekodi za Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania

Lakini JKT Queens waliomaliza nafasi ya pili msimu uliopita, nao wana nafasi kubwa ya kurejea kileleni. Pia, namna Yanga Princess ilivyotwaa ubingwa wa Samia Women Super Cup inaweza kuwa dalili ya ushindani wao msimu huu.

Kulingana na historia na mwenendo wa hivi karibuni, Simba Queens inaonekana kuwa na nafasi nzuri kutokana na uzoefu na wachezaji wenye ubora wa hali ya juu. Hata hivyo, JKT Queens na Yanga Princess zinaweza kuwapa ushindani mkali/Rekodi za Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania.

Mashabiki wa soka la wanawake wanatarajia msimu wa kusisimua na bado ni mapema kutabiri nani atatwaa ubingwa. Je, Simba Queens itaongeza taji lao la tano au JKT Queens itarejea kileleni? Au kutakuwa na mshindi mpya ambaye atavunja rekodi? Majibu yatapatikana mwishoni mwa msimu!

ANGALIA PIA: