Sakata la Dabi ya Kariakoo Juni 15, Tiketi za Machi 8 Zitatumika | Simba SC imetoa taarifa rasmi kwa wanachama wake, mashabiki na wananchi kwa ujumla kuthibitisha kuwa mchezo wa Kariakoo derby dhidi ya Yanga SC, mchezo wa 184 wa Ligi Kuu ya NBC, utachezwa Juni 15, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Katika taarifa hiyo, Simba imewahakikishia mashabiki wake kuwa tiketi zilizotumika kununua mechi hiyo ya Machi 8, 2025, ambazo hazikufanyika kama ilivyopangwa, zitakuwa halali kwa mechi hiyo ya Juni 15. Wale ambao bado hawajanunua tiketi wametakiwa kuwa tayari kuzipata mara tu Bodi ya Ligi itakapotangaza rasmi kuanza kwa mauzo.
Sakata la Dabi ya Kariakoo Juni 15, Tiketi za Machi 8 Zitatumika

Katika taarifa hiyo, Simba iliitaka TFF na Bodi ya Wakurugenzi ya Ligi kutoa ripoti ya uchunguzi wa kuvurugika kwa mechi ya ligi hiyo iliyopangwa kufanyika jioni ya Machi 7, 2025, pamoja na kuwachukulia hatua waliohusika na vurugu na uchochezi.
Klabu hiyo ilisisitiza kuwa kukosekana kwa ripoti na hatua madhubuti ni sawa na kuendelea uharamia unaotishia maendeleo ya soka la Tanzania ambalo limepata mafanikio makubwa katika miaka ya hivi karibuni.
CHECK ALSO:








Weka maoni yako