Simba Yapenya Kwenye Orodha ya Vilabu Bora Afrika Viwango vya CAF 2025

Simba Yapenya Kwenye Orodha ya Vilabu Bora Afrika Viwango vya CAF 2025 | Baada ya kufuzu kwa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF 2024/2025, klabu ya Simba SC ya Tanzania imepanda kwa kasi viwango vya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na sasa ni miongoni mwa klabu nne bora barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa na CAF, Simba SC imefikisha pointi 43, hatua iliyoiwezesha kupanda hadi nafasi ya nne kwenye orodha ya klabu bora Afrika. Hii ni mara ya kwanza kwa klabu kutoka Afrika Mashariki kuingia kwenye orodha kuu, ikionyesha ukuaji wa soka katika ukanda huu.

Simba Yapenya Kwenye Orodha ya Vilabu Bora Afrika Viwango vya CAF 2025

Simba Yapenya Kwenye Orodha ya Vilabu Bora Afrika Viwango vya CAF 2025
Simba Yapenya Kwenye Orodha ya Vilabu Bora Afrika Viwango vya CAF 2025

Orodha ya 10 Bora Afrika kwa Viwango vya CAF (2020–2025)

  1. πŸ‡ͺπŸ‡¬ Al Ahly β€” Pointi 78

  2. πŸ‡ΏπŸ‡¦ Mamelodi Sundowns β€” Pointi 57

  3. πŸ‡ΉπŸ‡³ Esperance de Tunis β€” Pointi 57

  4. πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Simba SC β€” Pointi 43

  5. πŸ‡²πŸ‡¦ RS Berkane β€” Pointi 42

  6. πŸ‡ͺπŸ‡¬ Zamalek SC β€” Pointi 42

  7. πŸ‡²πŸ‡¦ Wydad AC β€” Pointi 39

  8. πŸ‡ͺπŸ‡¬ Pyramids FC β€” Pointi 37

  9. πŸ‡©πŸ‡Ώ USM Alger β€” Pointi 37

  10. πŸ‡©πŸ‡Ώ CR Belouizdad β€” Pointi 36

Kupanda kwa Simba SC kunatokana na mafanikio yake ya mara kwa mara katika mashindano ya CAF katika miaka ya hivi karibuni. Klabu hiyo imekuwa ikishiriki mara kwa mara katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho na kufika hatua ya robo fainali na sasa nusu fainali jambo ambalo linaongeza pointi zake kulingana na mfumo wa pointi wa CAF.

CHECK ALSO: