Simba Yasajili Wachezaji Saba Wapya 2025/2026: Yawaaga Wachezaji 10. Simba Sports Club imekamilisha usajili wa wachezaji saba wapya hadi sasa ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake ya msimu wa 2025/2026 unaojumuisha Ligi Kuu ya NBC, Kombe la TFF na Ligi ya Mabingwa Afrika CAF.
Simba Yasajili Wachezaji Saba Wapya 2025/2026
Usajili huu unaonyesha dhamira ya klabu katika kuimarisha orodha yake ya mashindano ya ndani na kimataifa/Simba Yasajili Wachezaji Saba Wapya 2025/2026.
β Wachezaji Waliosajiliwa Mpaka Sasa:
-
Anthony Mligo β Beki wa kushoto, ametokea Namungo FC.
-
Mohamed Bajaber β Beki wa kati, raia wa Kenya.
-
Jonathan Sowah β Mshambuliaji hatari kutoka Ghana.
-
Hussein Daudi Semfuko β Kiungo mkabaji, chipukizi mwenye kipaji.
-
Morice Abraham β Kiungo mshambuliaji wa ubunifu mkubwa.
-
Rushine De Reuck β Beki wa kati anayemudu pia nafasi ya kiungo mkabaji, raia wa Afrika Kusini.
-
Alassane Maodo KantΓ© β Kiungo wa kati kutoka CA Bizertin (Tunisia), mwenye uzoefu wa kimataifa.
Wachezaji 10 Waliotemwa na Simba SC:
Katika kuhakikisha kikosi kinabaki imara na chenye ushindani, Simba SC imethibitisha kuachana na wachezaji 10, baadhi yao kwa uhamisho wa moja kwa moja na wengine kwa mkopo. Waliotajwa ni:
-
Che Malone
-
Debora Mavambo
-
Mohamed Hussein
-
Kelvin Kijili
-
Hussein Kazi
-
Augustine Okejepha
-
Valentin Nouma
-
Aishi Manula β Kipa namba moja wa muda mrefu.
-
Fabrice Ngoma
-
Omary Omary β Amepelekwa kwa mkopo kwenda Mashujaa FC.
Simba SC imesalia kuwa moja ya vilabu vya kulipwa vya soka Afrika Mashariki na Kati. Usajili huu mpya unaonyesha azma yao ya kuwania mataji ya ndani na kufuzu katika mashindano ya kimataifa.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako