Simba Yatinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB

Simba Yatinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB: Simba SC imefuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB (FA) baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bigman FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex katika hatua ya 16 Bora.

Simba Yatinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB

Matokeo ya Mchezo

🔹 Fainali: Simba SC 2-1 Bigman FC
⚽ Joshua Mutale 15’ (Simba SC)
⚽ Leonel Ateba 30’ (P) (Simba SC)
⚽ Henock 45’ (Bigman FC)

Simba Yatinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB
Simba Yatinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB

Simba SC walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Joshua Mutale dakika ya 15. Dakika 15 baadaye, Leonel Ateba aliongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti. Bigman FC ilijibu kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa bao la Henock dakika ya 45.

Kwa ushindi huo, Simba SC inasonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB (FA) na sasa inasubiri droo ya robo fainali kuamua mpinzani wake mwingine.

CHECK ALSO: