Simba Yazuiwa Kufanya Mazoezi Benjamin Mkapa Kabla ya Kariakoo Derby | Timu ya Simba SC imewasili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini imezuiwa kuingia na kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Yanga SC. Watu wanaodai kuwa ni makomandoo wa Yanga waliwazuia Simba kuingia uwanjani.
Simba Yazuiwa Kufanya Mazoezi Benjamin Mkapa Kabla ya Kariakoo Derby
Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), Yanga SC watakuwa wenyeji wa Simba SC kesho saa 1:00 usiku. katika mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
Taarifa kutoka kwa viongozi wa Simba SC zinaeleza kuwa timu hiyo ilikuwa ifanye mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini viongozi wa uwanja huo wameeleza kuwa hawana taarifa za kuruhusu timu yoyote kufanya mazoezi hapo leo.

Baada ya kuzuiliwa, kikosi cha Simba SC kiliondoka uwanjani saa 3:00 usiku. bila kufanya mazoezi. Hali hii inazua mjadala mkubwa kabla ya mechi ya kesho, huku mashabiki wa timu zote mbili wakisubiri kwa hamu kile kinachotarajiwa kuwa moja ya mechi kali zaidi msimu huu.
Sababu zakikachero
Sababu maalum zaidi ni kwamba mbona miaka yote hawakuwa wakienda kufanya mazoezi ya mwisho hivyo hawawezi kuwaruhusu, kitendo cha kumzuia Simba kufanya mazoezi ni kuvunja kanuni na kumnyima haki Mgeni wa mchezo huo ambaye alitaka kufanya mazoezi ya mwisho muda sahihi kuendana na kesho.
Kufuatia Simba kuzuia tangu saa moja kuingia uwanjani imelazimika Wachezaji ambao wapo kwenye mfungo wa Ramadhan na Kwaresma kufuturu kwenye Bus huku wakiondoka rasmi uwanja wa Mkapa saa tatu usiku huu baada ya kushindwa kuingia uwanjani. Simba Yazuiwa Kufanya Mazoezi Benjamin Mkapa Kabla ya Kariakoo Derby.
ANGALIA PIA:
Weka maoni yako