Singida Black Stars Vs Yanga: Mechi ya Uzinduzi wa Airtel Stadium Machi 24 | Klabu ya Singida Black Stars itafungua rasmi uwanja wake mpya, Uwanja wa Airtel, Jumatatu Machi 24, 2025. Kusherehekea tukio hilo, Singida KE itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga SC.
Mechi hii ya kihistoria itaanza saa 10:00 Jioni na itaonyeshwa moja kwa moja kwenye vituo mbalimbali vya televisheni na digitali. Yanga SC, ambayo itaondoka Dar es Salaam Machi 22 kupitia usafiri wa SGR, inalenga kuwa timu ya kwanza kushinda katika uwanja huo mpya.
Mashabiki wa soka wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo maalum, ambayo pia itatoa fursa kwa wachezaji wa pande zote mbili kuonyesha ujuzi wao kabla ya kurejea kwenye mchezo wa ushindani.

CHECK ALSO:
- Kikosi cha Yanga Kuondoka Dar es Salaam Machi 22 kwa Usafiri wa SGR
- Michael Olunga Kenya Bado Ina Nafasi ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026
- Kocha Salum Mayanga Ajiunga na Mashujaa FC Akitokea Mbeya City
- Simba SC vs Al Masry Robo Fainali CAF kupigwa April 02 na 09, 2025
- Ratiba ya Robo Fainali CAF Champions League na Confederation Cup 2024-25
Weka maoni yako