Singida Black Stars Wamtaka Amankona, Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji

Singida Black Stars Wamtaka Amankona, Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji | Klabu ya Singida Black Stars ya Tanzania imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji mahiri Mghana Stephen Amankona (25) mchezaji wa Berekum Chelsea.

Habari za uhakika zimeeleza kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanaendelea, na tayari mchezaji huyo ametajwa kuwa nyota wa Singida Black Stars kwa msimu wa 2025/2026.

Singida Black Stars Wamtaka Amankona, Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji

Stephen Amankona ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufumania nyavu, akiwa ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Ghana kwa misimu miwili mfululizo:

Singida Black Stars Wamtaka Amankona, Kuimarisha Safu ya Ushambuliaji

  • Msimu wa 2024/25: Mabao 15

  • Msimu wa 2023/24: Mabao 19

Uwezo wake wa kuongoza mashambulizi umemfanya alengwe na klabu kadhaa za Afrika. Singida Black Stars inaamini kusajiliwa kwake kutaimarisha kwa kiasi kikubwa kikosi chao hasa katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

CHECK ALSO:

  1. Florent Ibenge Karibu Kujiunga na Azam kama Kocha Mkuu Mpya
  2. Hatma ya Maxi Nzengeli Yanga, Mkopo Mpya au Ofa Maniema
  3. Raundi ya 29 NBC Ligi Kuu, Mechi Zote Nane Kupigwa Saa 10:00 Jioni Juni 18
  4. Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara 2024/2025