Tabora United vs Yanga, Je Wananchi Watalipa Kisasi au Ubabe Utaendelea?

Tabora United vs Yanga, Je Wananchi Watalipa Kisasi au Ubabe Utaendelea? Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Tabora United dhidi ya Yanga SC unazidi kupamba moto huku maandalizi yakiendelea kwa kasi kuelekea mchezo huo utakaopigwa Aprili 2, 2025 saa 10:15 jioni. Mashabiki wa soka nchini wanasubiri kwa hamu kuona iwapo Yanga SC italipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1 katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

Tabora United vs Yanga, Je Wananchi Watalipa Kisasi au Ubabe Utaendelea?

Kuwasili kwa viongozi wa Yanga SC akiwemo Meneja Habari na Mawasiliano Ally Kamwe na Mkurugenzi wa Masoko na Uanachama Ibrahim Samwel mjini Tabora na “kijiji” chao cha Wananchi kumeongeza hamasa ya mchezo huo. Hii ni ishara kuwa klabu hiyo imechukua hatua zinazofaa kuhakikisha mashabiki wake wanapata sapoti ya kutosha kushuhudia mechi hiyo ya kusisimua.

Tabora United vs Yanga, Je Wananchi Watalipa Kisasi au Ubabe Utaendelea?
Tabora United vs Yanga, Je Wananchi Watalipa Kisasi au Ubabe Utaendelea?

Kwa upande wa Yanga SC, kocha Hamdi Miloud na kikosi chake wanajua ushindi katika mechi hii ni muhimu si kwa ajili ya kulipiza kisasi tu bali pia kuendeleza nia ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC. Kwa upande wao, Tabora United wana hamu ya kudhihirisha ushindi wao wa mzunguko wa kwanza haukuwa wa kusuasua na watashuka uwanjani wakiwa na lengo la kuendeleza ubabe dhidi ya mabingwa hao watetezi.

Je, Yanga SC wanaweza kurejesha heshima yao kwa kulipiza kisasi, au Tabora United itabaki kuwa mwiba mchungu kwa Wananchi? Mashabiki wa soka wanasubiri kwa hamu kuona jinsi mambo yatakavyokuwa kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

CHECK ALSO: