Tetesi za Fei Toto Kurudi Yanga Ipo Hivi, Simba Waonyesha Nia Pia: Yanga SC Yamtaka Feisal Salum Fei Toto Kama Mrithi wa Aziz Ki. Young Africans SC (Yanga) imeanza rasmi mazungumzo ya kumrejesha kiungo wake wa zamani, Feisal Salum “Fei Toto,” ambaye kwa sasa anakipiga Azam FC.
Tetesi za Fei Toto Kurudi Yanga Ipo Hivi, Simba Waonyesha Nia Pia
Taarifa zinaeleza kuwa tayari uongozi wa Yanga umeshawasilisha ofa kubwa zaidi ya iliyotolewa na Simba SC na Azam FC lengo likiwa ni kumshawishi kiungo huyo kurejea Jangwani.
Hatua hii imekuja wakati Yanga ikiandaa mbadala wa kiungo wake nyota Stephane Aziz Ki anayetarajiwa kujiunga na miamba ya soka ya Morocco Wydad Casablanca mwishoni mwa msimu wa 2024/2025.
Changamoto za usajili wa Fei Toto:
Licha ya nia njema ya kumrejesha Fei Toto, changamoto bado zipo kutokana na namna alivyoihama klabu hiyo mara ya kwanza. Hata hivyo, Yanga SC inadaiwa iko tayari kufanya jitihada kubwa kurejesha mahusiano na kiungo huyo kwa manufaa ya timu.

Fei Toto bado ni mchezaji wa Azam FC, na anatajwa kuwa miongoni mwa viungo wenye kiwango bora katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu.
Mazungumzo kati ya Yanga na wawakilishi wake yanaendelea, huku wakisubiri kwa hamu kuona kama dili hilo litakamilika kabla ya dirisha la usajili kufunguliwa rasmi.
Uongozi wa Yanga unaamini kurejea kwa Fei Toto kutaimarisha safu ya kiungo hasa kuelekea mashindano ya kimataifa msimu ujao kutokana na tetesi za kuondoka kwa kiungo wao mahiri Aziz KI.
Iwapo Fei Toto atakubali kurejea Yanga, basi itakuwa moja ya usajili mkubwa utakaotikisa dirisha lijalo, huku pia ikionekana kuwa suluhisho sahihi la pengo litakaloachwa na Aziz Ki kama atatimikia Morocco kama tetesi zinavyosema. Yanga SC Yamtaka Feisal Salum Fei Toto Kama Mrithi wa Aziz Ki.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako