TPLB Yaitolea Ufafanuzi Yanga Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba

TPLB Yaitolea Ufafanuzi Yanga Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba | Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imejibu rasmi malalamiko ya Yanga SC kuhusu mechi yao dhidi ya Simba SC iliyofutwa Machi 16, 2025.

Katika barua yenye kumbukumbu namba TPLB/2024/625, TPLB imefafanua kuwa hakuna msingi wa kisheria wa kuipa Yanga pointi tatu, huku ikitoa sababu kuu kumi za uamuzi wake huo/TPLB Yaitolea Ufafanuzi Yanga Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba.

TPLB Yaitolea Ufafanuzi Yanga Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba

TPLB Yaitolea Ufafanuzi Yanga Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba
TPLB Yaitolea Ufafanuzi Yanga Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba

Sababu Kuu Zinazotolewa na TPLB

  1. Mchezo Ulighairishwa Mapema: TPLB ilighairisha mchezo huo majira ya saa 8 mchana, na baada ya uamuzi huo hakukuwa na maafisa wa mchezo uwanjani, zaidi ya watu wa usalama pekee.

  2. Taratibu za Mchezo Hazikufanyika: Kwa mujibu wa Kanuni ya 17, ili timu ipewe alama tatu, lazima taratibu rasmi za mchezo kama ukaguzi wa timu ufanyike. Hii haikufanyika.

  3. Sababu za Kikanuni Ndiyo Zilizoghairisha Mchezo: TPLB ilieleza kuwa Simba SC haikugomea mchezo, bali Kamati ya Masaa 72 iliamua kuufuta kutokana na changamoto mbalimbali za kikanuni.

  4. Simba SC Haikuvunja Kanuni kwa Kutotoa Taarifa ya Mazoezi: TPLB imefafanua kuwa hakuna kanuni inayoitaka klabu mgeni kutoa taarifa kwa klabu mwenyeji kuhusu mazoezi yao. Hili ni mwongozo wa TPLB pekee, si kanuni rasmi.

  5. Masuala ya Usalama Yalizingatiwa: Mchezo ulighairishwa kutokana na tuhuma za rushwa, vitisho, na changamoto za kiusalama, ambazo zingehatarisha usalama wa mchezo kabla, wakati, na baada ya mechi.

  6. Yanga SC Kulazimisha Kufika Uwanjani Ni Kinyume na Kanuni: Kwa mujibu wa Kanuni ya 47(18), Yanga SC ilikiuka taratibu kwa kupeleka timu uwanjani baada ya mchezo kufutwa, jambo ambalo linaonekana ni kupingana na mamlaka.

  7. Gharama za Yanga Zitashughulikiwa Kikanuni: TPLB imehakikishia Yanga SC kuwa gharama walizoingia zitazingatiwa kulingana na kanuni za ligi.

  8. Ratiba Mpya ya Derby Kutangazwa Rasmi: TPLB imewatakia Yanga SC maandalizi mema na kuahidi kutangaza tarehe mpya ya mchezo wa Derby kati yao na Simba SC.

Kwa mujibu wa majibu ya TPLB, Yanga SC haitapewa pointi tatu kutokana na kufutwa kwa mchezo huo, kwa kuwa hakuna kanuni inayoruhusu kitendo hicho/TPLB Yaitolea Ufafanuzi Yanga Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba.

Masuala ya usalama, taratibu za udhibiti, na maamuzi ya Kamati ya Saa 72 yalichangia maamuzi haya. Mashabiki wa soka sasa wanasubiri kutangazwa rasmi kwa tarehe mpya ya pambano kati ya wapinzani wa jadi Yanga SC na Simba SC.

CHECK ALSO: