TPLB Yakanusha Taarifa za Yanga Kudai Alama 3, Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Dabi ya Kariakoo | Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) Karim Boimanda amekanusha taarifa zilizoenea mtandaoni kuwa Yanga SC imewasilisha barua ya kutaka pointi tatu kwa ajili ya mchezo wa Kariakoo derby uliopangwa kufanyika Machi 8, 2025.
TPLB Yakanusha Taarifa za Yanga Kudai Alama 3, Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Dabi ya Kariakoo
Katika maelezo yake, Boimanda alieleza kuwa hakuna barua rasmi kutoka Yanga SC kuhusiana na madai hayo. Pia alikiri kuwa TPLB inapata shida katika kupanga tarehe mpya ya mechi hiyo kutokana na ratiba ya mashindano mbalimbali yanayoendelea.
“Tunaendelea kujitahidi kutafuta tarehe mwafaka ya mechi hii muhimu ili mashabiki wa timu zote mbili wafurahie burudani waliyokosa Machi 8,” Boimanda alisema na kuwataka mashabiki kuwa watulivu wakati juhudi zikiendelea.
Mchezo wa Kariakoo derby kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC ni kati ya mechi muhimu na za kusisimua katika soka la Tanzania, hivyo tangazo la tarehe mpya litasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu zote mbili. Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi!
CHECK ALSO:
Weka maoni yako