Usajili Simba Leo, Wachezaji Wanaotakiwa Msimbazi

Usajili Simba Leo, Wachezaji Wanaotakiwa Msimbazi | Dirisha Kubwa la Usajili Ligi Kuu Bara 2025/2026: Simba Waanza Harakati za Usajili.

Kipindi cha usajili wa dirisha kubwa Ligi Kuu Tanzania Bara kinakaribia kufunguliwa, tayari vigogo wa soka nchini, Simba SC na Yanga SC, wameanza kuweka mikakati ya kuimarisha vikosi vyao kuelekea msimu ujao wa mashindano ya kimataifa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, kuna vuguvugu la ndani kati ya klabu hizo mbili kubwa nchini, zikihusisha kusaka wachezaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), taifa lenye vipaji vingi vya soka.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara inathibitisha kuwa Simba na Yanga zitaiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025/2026, huku Singida Black Stars na Azam FC zikitarajiwa kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Usajili Simba Leo, Wachezaji Wanaotakiwa Msimbazi
Usajili Simba Leo, Wachezaji Wanaotakiwa Msimbazi

Usajili Simba Leo, Wachezaji Wanaotakiwa Msimbazi

Waliosajiliwa Mpaka sasa Simba

  1. Morice Abraham – Kutoka FK Spartak Subotica
  2. Rushine De Reuck (29) – Mamelodi Sundowns
  3. Charles Daud Semfuko 🇹🇿 – Coastal Union
  4. Anthony Mligo – Coastal Union
  5. Alassane Kanté – Kutoka CA Bizertin
  6. Mohamed Bajaber – kutoka Police Kenya FC
  7. Jonathan Sowah – Kutoka Singida Black Stars
  8. Naby Camara – Kutoka AS Kaloum
  9. Yakoub Suleiman – Kutoka JKT Tanzania
  10. Wilson Nangu – Kutoka JKT Tanzania

Kuhakikisha mafanikio katika mashindano ya kimataifa kunahitaji uwekezaji wa mapema katika usajili wa nguvu, unaozingatia ubora wa wachezaji, uzoefu wao, na uwezo wa kushindana kwa kiwango cha juu. Kwa hiyo, Simba na Yanga zinasaka vipaji kutoka DRC, taifa ambalo limekuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika kwa kuzalisha wachezaji wa kiwango cha juu.

CHECK ALSO: