Usajili wa Balla Moussa Conte Yanga, Simba na Azam | Soko la usajili barani Afrika linaendelea kushika kasi, huku klabu kubwa za Tanzania, Yanga SC, Simba SC, na sasa Azam FC zikiwania saini ya mshambuliaji wa Guinea, Balla Moussa Conte, anayekipiga katika klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, klabu zote tatu zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo, lakini kila moja inakabiliwa na changamoto tofauti katika mchakato huo.
Usajili wa Balla Moussa Conte Yanga, Simba na Azam
YANGA SC YAFIKIA MAKUBALIANO NA SFAXIEN
Tayari Yanga SC imethibitisha kufanya malipo ya awali kwa CS Sfaxien kama sehemu ya makubaliano ya kumpata Balla Moussa Conte. Taarifa zinaeleza kuwa hakuna pingamizi kwa klabu hizo mbili, lakini bado kuna vikwazo katika makubaliano binafsi kati ya Yanga na mchezaji huyo.
Yanga kwa sasa inaendelea na kazi ya kukamilisha makubaliano binafsi na kuhakikisha mchezaji huyo anajiunga rasmi kabla ya tarehe ya mwisho ya usajili.
SIMBA SC YAONYESHA NIA, LAKINI OFA YAKE BADO HAIJIBIWA.
Kwa upande wa Simba SC, taarifa zinaeleza kuwa tayari wameshawasilisha ofa kwa CS Sfaxien, lakini bado hawajapata majibu. Hata hivyo, mchezaji huyo na Simba hawajaweka pingamizi lolote; inaripotiwa kuwa pande zote mbili hudumisha uelewa mzuri.

Hii inaashiria kuwa iwapo CS Sfaxien itakubali ofa ya Simba, kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kujiunga na Wekundu wa Msimbazi kwa masharti waliyokubaliana.
🔵 AZAM FC YAINGIA KWENYE MBIO ZA SAINI
Katika hali ya kustaajabisha, Azam FC nayo imeingia kwenye mbio za kutafuta huduma ya Balla Moussa Conte. Klabu hiyo imeweka wazi kuwa iko tayari kuwasilisha ofa rasmi, na kuifanya kuwa mshindani mpya katika sakata hili la uhamisho.
Hii inafanya idadi ya klabu za Tanzania zinazowania saini ya mchezaji huyo kufikia tatu, na huenda ushindani ukaongeza thamani ya mchezaji na kufanya uamuzi wa mwisho kuwa mgumu zaidi.
CHECK ALSO:






Weka maoni yako