Viingilio vya Mechi ya Simba vs Al Masry Vyatangazwa | Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally alitangaza kupatikana kwa viingilio vya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC na Al Masry ya Misri. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Viingilio vya Mechi ya Simba vs Al Masry Vyatangazwa
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, viingilio vya mchezo huo ni kama ifuatavyo:

Mzunguko – TSH 5,000
Orange – TSH 10,000
VIP C – TSH 15,000
VIP B – TSH 30,000
VIP A – TSH 40,000
Platinum – TSH 150,000
Tanzanite – TSH 250,000
Ahmed Ally pia alithibitisha kuwa tiketi tayari zimeanza kuuzwa, na mashabiki wanahimizwa kuzinunua mapema ili kuepuka usumbufu wowote siku ya mechi.
Umati mkubwa wa Simba SC unatarajiwa kuisapoti timu yao katika mechi hiyo muhimu ya michuano ya kimataifa.
“Mechi hii tunataka kuingiza mashabiki kati ya 50,000 hadi 60,000 hivyo tutafanya hamasa kubwa, mtaa kwa mtaa ili kuwahamasisha Wanasimba kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo muhimu. Safari hii tutatembelea matawi mengi sababu tunataka watu wengi waje uwanjani.”- Semaji Ahmed Ally.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako