Viongozi wa Matawi ya Yanga Dodoma Wataka Wallace Karia Aombe Radhi

Viongozi wa Matawi ya Yanga Dodoma Wataka Wallace Karia Aombe Radhi | Kugoma Kurudiana Mechi dhidi ya Simba SC.

Viongozi wa tawi la Young Africans SC (Yanga SC) na wazee wa klabu hiyo mkoani Dodoma wametoa kauli nzito wakimtaka Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia kuomba radhi hadharani kutokana na kauli aliyoitoa kufuatia kuahirishwa kwa mchezo wa watani wa jadi Yanga SC na Simba SC.

Katika mkutano wao na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Machi 18, 2025 viongozi na wazee hao wameeleza kutoridhishwa kwao na maamuzi yaliyochukuliwa na kusema wamepoteza imani na uongozi wa TFF chini ya Wallace Karia/Viongozi wa Matawi ya Yanga Dodoma Wataka Wallace Karia Aombe Radhi.

Viongozi wa Matawi ya Yanga Dodoma Wataka Wallace Karia Aombe Radhi

Msimamo wa viongozi wa Yanga Dodoma

Mzee Abdalah Mtosa Ally wa tawi la Chang’ombe alisisitiza kuwa mechi hiyo isirudiwe, kwani Machi 8 ndiyo tarehe sahihi.

Kwa upande wake, Bernard Mtengwa, mmoja wa wazee wa Yanga, alisema:

Viongozi wa Matawi ya Yanga Dodoma Wataka Wallace Karia Aombe Radhi
Viongozi wa Matawi ya Yanga Dodoma Wataka Wallace Karia Aombe Radhi

“Mimi kama mzee wa Yanga Dodoma, kwa masikitiko makubwa, hatuna imani na Karia kwani tunajua wazi hana mapenzi ya dhati na Yanga. Niwaombe viongozi wa juu kutoruhusu mechi hiyo kufanyika tena. Kama ni faini tuko tayari kulipa, lakini siyo kurudia mechi na Simba.”

Bodar Awadhi Ahmed, mzee mwingine wa Yanga, alieleza kuwa uamuzi wa kuahirisha mechi hiyo umewachanganya mashabiki wa soka nchini, huku wengi wakipinga uwezekano wa kuchezwa tena.

Mashtaka dhidi ya Wallace Karia

Viongozi hao walidai Wallace Karia ameonyesha upendeleo na kuwadhalilisha mashabiki wa Yanga kwa kauli zake. Walisisitiza kuwa hawana imani naye tena na kumtaka aombe msamaha hadharani.

“Sisi msimamo wetu ni kutokurudia mechi. Kwanza Rais wa TFF ametudhalilisha Wanayanga, na kama ameshindwa mpira, arudi kwenye taaluma yake, kwani tunaijua,” walieleza kwa msisitizo.

Kwa upande wake, Mratibu wa Yanga Dodoma, Elisha Ngwando, alimtaka Karia kuwaomba radhi wanachama wa Yanga na wanamichezo kwa ujumla kwa maamuzi aliyofanya na kauli alizotoa/Viongozi wa Matawi ya Yanga Dodoma Wataka Wallace Karia Aombe Radhi.

“Watu wametumia gharama kubwa, wengine wamelipia matangazo kwa ajili ya mechi hiyo,” alisema Ngwando.

CHECK ALSO: