Wydad AC Yaitandika CS Saint-Laurent 7-0 Katika Mchezo wa Kirafiki | Katika mechi ya kirafiki iliyochezwa leo, Wydad AC ya Morocco iliibuka na ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Club de Soccer Saint-Laurent.
Mechi hiyo ilikuwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA 2025, ambalo limepangwa kuanza Juni 14.
Mchezaji bora wa mechi hiyo alikuwa Selemani Mwalimu, aliyefunga bao moja na kutoa pasi tatu za mabao. Mwalimu alitoa pasi mbili za mabao kwa mshambuliaji Samuel Obeng na nyingine ya Stéphane Aziz Ki.
Wydad AC Yaitandika CS Saint-Laurent 7-0 Katika Mchezo wa Kirafiki

Wafungaji wa Mabao ya Wydad AC Leo:
⚽️⚽️⚽️ Samuel Obeng (hat-trick)
⚽️ Stephane Aziz Ki
⚽️ Selemani Mwalimu
⚽️ Mohamed Rayhi
⚽️ Omar Al Somah
Ushindi huu unawapa matumaini mashabiki wa Wydad AC kwa maandalizi ya timu hiyo, huku wachezaji wakionyesha kiwango cha juu hasa wale walio kwenye kikosi rasmi cha FIFA.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako