Yanga Matatani Ligi Kuu, Nini Kitatokea Wasipocheza Juni 15 | Yanga SC iko hatarini kupoteza pointi 15 kwa kutojitokeza uwanjani.
Yanga SC ipo kwenye hatari kubwa ya kupoteza pointi 15 baada ya kusisitiza msimamo wake wa kutocheza mchezo wa watani wa jadi Simba SC. Endapo mechi hiyo haitachezwa kwenye uwanja huo, uamuzi huu unaweza kuipa Simba nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025.
Yanga Matatani Ligi Kuu, Nini Kitatokea Wasipocheza Juni 15
Kwa mujibu wa Kanuni ya 31 ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Toleo la 2024, Ibara ya 1 (1.3), timu yoyote itakayoshindwa kufika uwanjani bila sababu za msingi zinazokubalika na TFF au Bodi ya Ligi (TPLB) itakabiliwa na adhabu kali ya pointi 15. Adhabu hii inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa nafasi ya Yanga kwenye msimamo wa ligi, si kwa ubingwa tu bali hata ile ya kumaliza nafasi ya pili, inayoipa tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Katika kipengele hicho, pia imeelezwa kuwa:
Timu itatozwa faini ya shilingi milioni tano (TSh 5,000,000), ambapo milioni mbili na laki tano (2,500,000) ni kwa ajili ya Bodi ya Ligi, na kiasi kama hicho kwa timu pinzani.
Timu inapaswa kulipa fidia ya uharibu au maandalizi.
Viongozi waliohusika wanaweza kufungiwa kwa miezi 12.
Ikiwa timu itakuwa na alama pungufu ya 15, itapewa alama hasi na hata msimu ujao itaanza na alama hizo hasi.
Pia itapoteza haki ya mapato ya mchezo husika.
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, lakini endapo itapokwa pointi na Azam FC kufanya vizuri katika mechi zao zilizosalia, kuna uwezekano wa klabu hiyo kupoteza nafasi ya pili na hivyo kukosa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako