Yanga Princess Mabingwa wa Samia Womens Super Cup 2025

Yanga Princess Mabingwa wa Samia Womens Super Cup 2025 | Timu ya Yanga Princess ya Wanawake imetwaa ubingwa wa Kombe la Samia kwa Wanawake 2025 baada ya kuifunga JKT Queens mabao 3-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Yanga Princess Mabingwa wa Samia Womens Super Cup 2025

Matokeo ya mwisho

Queens 0-3 Princess Yanga
⚽ Aregash Kalsa
⚽ Jeannine Mukandayisenga (mabao mawili)

Ushindi huu unaifanya Yanga Princess kuwa mabingwa wa mashindano haya kwa msimu huu, wakionyesha kiwango cha juu kwenye fainali dhidi ya wapinzani wao wakuu.

Yanga Princess Mabingwa wa Samia Womens Super Cup 2025
Yanga Princess Mabingwa wa Samia Womens Super Cup 2025

Mshindi wa tatu

Katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu, Simba Queens ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate Princess.

Simba Queens 2-1 Fountain Gate Princess
⚽ Jentrix Shikangwa
⚽ Wincate Kaari
⚽ Winnie Gwatenda

Michuano ya Samia Women’s Super Cup 2025 imedhihirisha ushindani wa hali ya juu katika soka la wanawake wa Tanzania. Yanga Princess walionyesha ubora wao kwa kutwaa taji hilo kwa kishindo, huku Simba Queens wakimaliza nafasi ya tatu. Mashindano haya yanaendelea kuleta msisimko na kusukuma maendeleo ya soka la wanawake nchini.

ANGALIA PIA: