Yanga vs Simba Juni 15, Kariakoo Derby ya 37 za Mwisho, Simba Yaongoza kwa Ushindi Jumapili | Kariakoo Derby Juni 15, 2025: Itakuwa Mchezo wa 37 Kati ya Yanga na Simba Kukutana Tangu 1965.
Mchezo wa watani wa jadi unaofahamika kwa jina la Kariakoo derby kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC utapigwa Jumapili ya Juni 15, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Hii itakuwa mara ya 37 kwa wababe hao wawili wa soka la Tanzania kukutana Jumapili moja tangu 1965.
Yanga vs Simba Juni 15, Kariakoo Derby ya 37 za Mwisho, Simba Yaongoza kwa Ushindi
Katika michezo 36 ya awali ambayo imechezwa siku ya Jumapili:
Simba SC inaongoza kwa ushindi kwa kufanikisha mara 9,
Yanga SC imeshinda mara 7 tu,
Wakati michezo mingine 20 ikimalizika kwa sare.
Pambano hili la kihistoria linatarajiwa kuwa vuta nikuvute kutokana na umuhimu wake katika mapambano ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, pamoja na historia ndefu ya upinzani mkali baina ya timu hizo mbili kongwe nchini.
Kando na upinzani wa jadi, mechi hii inaweza kuwa na athari kubwa kwenye mkondo wa michuano ya 2024/2025, haswa ikiwa moja ya timu itakuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa au kumaliza katika nafasi ya kwanza.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako