Yanga Yaenda CAS Kupinga Uamuzi wa TPLB na TFF Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba | Yanga SC yafungua kesi Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kufuatia kutoridhishwa na uamuzi wa TPLB na TFF.
Yanga Yaenda CAS Kupinga Uamuzi wa TPLB na TFF Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba
Yanga SC imefungua kesi Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kufuatia kutoridhishwa na majibu ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu kufutwa kwa mechi yake dhidi ya Simba SC.
Awali Yanga SC ilitarajiwa kupokea pointi tatu kutokana na mechi ya Kariakoo kufutwa, lakini TPLB ikafafanua kuwa hakuna kanuni inayotoa moja kwa moja pointi kwa timu katika mazingira hayo.
Sababu za Yanga SC kwenda CAS
- Yanga SC haijaridhishwa na maelezo yaliyotolewa na TPLB na TFF kuhusu sababu za kuahirishwa kwa mechi dhidi ya Simba SC.
- Wanapinga uamuzi wa kutopata pointi tatu, kwani wanaamini walipaswa kushinda mechi hiyo.
- Wanataka CAS ichunguze maamuzi ya TPLB na TFF na kuyapatia ufumbuzi wa haki.

Yanga SC Yasusia mechi ya marudiano
Pamoja na kukata rufaa CAS, Yanga SC imeamua kutocheza mechi nyingine ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba SC hadi hapo uamuzi wa rufaa yake utakapojulikana. Hii ina maana mechi ya Kariakoo derby inaweza kubaki katika hali ya sintofahamu hadi CAS itakapofanya uamuzi rasmi.
Uamuzi wa Yanga SC kukata rufaa CAS ni ishara ya kutoridhishwa kwao na uamuzi wa mamlaka ya soka Tanzania. Mashabiki wa soka wanasubiri kwa hamu uamuzi wa CAS, utakaoamua hatima ya mechi hii muhimu ya ligi/Yanga Yaenda CAS Kupinga Uamuzi wa TPLB na TFF Kuhusu Mchezo Dhidi ya Simba.
Je, CAS itaipa Yanga SC pointi tatu au itasimamia uamuzi wa TPLB na TFF? Endelea kufuatilia habari zaidi kuhusu sakata hili.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako