Yanga Yaingia Uwanjani Mkapa, Wachezaji Waanza Mazoezi | Katika hali inayoendelea kuzua mvutano, kikosi cha Yanga SC kimewasili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mechi ya Kariakoo derby, kikifanikiwa kuingia moja kwa moja bila kufungwa.
Yanga Yaingia Uwanjani Mkapa, Wachezaji Waanza Mazoezi
Ripoti hiyo inasema:
- Basi la Yanga SC halikupitia lango kuu la uwanja, lakini timu tayari imeshaingia na mara moja wachezaji wake wakaanza kupasha moto.
- Hali hii imekuja huku kukiwa na sintofahamu ya hatima ya mchezo huo, kufuatia uamuzi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kuahirisha mchezo huo leo.
📍 Benjamin Mkapa Stadium. 🤩🔰
#NBCPremierLeague #TheClubAboveAll#DaimaMbeleNyumaMwiko pic.twitter.com/j0QWkwlQhQ— Young Africans SC English (@YoungAfricansEN) March 8, 2025
Kwa sasa wachezaji wa Young Africans wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo licha ya kuwepo kwa taarifa za kuahirishwa kwake. Tunasubiri taarifa zaidi kutoka kwa mamlaka husika kuhusu mwelekeo wa mchezo huu na iwapo utaendelea au la.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako