Zawadi ya Bingwa Kombe la CRDB Federation Cup 2025 | Pesa za zawadi kwa mshindi wa Kombe la CRDB, michuano inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimebaki kuwa shilingi milioni 50, kiasi sawa na kile kilichotolewa na Azam Media katika michuano iliyopita.
Zawadi ya Bingwa Kombe la CRDB Federation Cup 2025
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, hakuna mabadiliko ya kiwango alichopokea mshindi wa kombe hilo, licha ya matarajio kutoka kwa wadau na mashabiki kuwa fedha za zawadi zinaweza kuongezeka kufuatia mabadiliko ya wadhamini kutoka Azam Media kwenda Benki ya CRDB.
TFF haijatoa mawasiliano yoyote rasmi, kwa maandishi au vinginevyo, kwa vilabu kuhusu ongezeko la fedha za zawadi. Hali hii imezua wasiwasi miongoni mwa wanachama wa klabu na wadau wa soka ambao walitarajia kuwepo kwa mfadhili mpya kungefungua milango ya motisha kwa washiriki wa mashindano hayo.
Ni vyema vyombo husika hasa TFF na wadhamini vihakikishe uwazi na taarifa za kutosha kwa vilabu na wananchi kuhusu suala la fedha za zawadi hasa linapokuja suala la mashindano ya ndani yenye uwezo wa kukuza vipaji na kuongeza ushindani.

Udhamini wa CRDB kwa TFF
Kumekuwa na sintofahamu katika sekta ya michezo Tanzania kufuatia hali ya fedha za zawadi ya mshindi wa kombe la CRDB kubaki shilingi milioni 50 sawa na zile zilizotolewa na Azam Media licha ya kuwepo kwa mkataba mpya wa udhamini kati ya Benki ya CRDB na TFF wenye thamani ya shilingi bilioni 3.759 kwa miaka mitatu.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, makubaliano hayo yanasababisha TFF kupokea takriban shilingi bilioni 1.253 kila mwaka kutoka kwa mfadhili mpya. Hata hivyo, fedha za zawadi kwa mshindi wa Kombe la CRDB hazijaongezwa na hivyo kuzua maswali mengi kuhusu matumizi ya fedha hizo.
Licha ya matarajio kuwa ongezeko la udhamini lingeboresha fedha za zawadi na maandalizi ya mashindano, TFF haijatoa taarifa za kina kuhusu matumizi ya fedha hizo wala kueleza ni kwa nini fedha za zawadi kwa mshindi hazijaongezwa. Zaidi ya hayo, hakuna barua rasmi iliyotumwa kwa vilabu kuhusu suala hili.
Wadau wa michezo wameeleza kusikitishwa kwao na kueleza kuwa huu ni wakati ambao TFF ilipaswa kuonyesha uwazi na kuwapa motisha wachezaji kwa kuongeza fedha za zawadi. Ikizingatiwa kuwa Kombe la CRDB ni shindano rasmi la kitaifa, pesa ya zawadi ya Euro milioni 50 inaonekana ndogo kwa kiwango hicho cha udhamini.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako