Dube Mchezaji Bora wa Februari Ligi Kuu NBC 2024/25

Dube Mchezaji Bora wa Februari Ligi Kuu NBC 2024/25 | MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Prince Mpumelelo Dube ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Februari wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2024/25 NBC. Dube aliibuka kidedea baada ya kuwabwaga wachezaji wengine waliokuwa wakiwania tuzo hiyo akiwemo Stephanie Aziz Ki wa Yanga SC na Selemani Bwenzi wa KenGold FC.

Dube Mchezaji Bora wa Februari Ligi Kuu NBC 2024/25

Mchango wa Prince Dube kwa Yanga SC

Februari, Prince Dube alionyesha kiwango bora kwa Yanga SC, akifunga mabao matano na kutoa pasi tano za mabao katika michezo saba aliyocheza. Chini ya uongozi wa kocha Miloud Hamdi, Yanga SC ilipata matokeo mazuri kwa kushinda mechi sita na kutoa sare moja, hivyo kujiimarisha kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi hiyo.

Dube Mchezaji Bora wa Februari Ligi Kuu NBC 2024/25
Dube Mchezaji Bora wa Februari Ligi Kuu NBC 2024/25

 

Miloud Hamdi ameteuliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi Februari

Mbali na Dube, Kocha wa Yanga SC, Miloud Hamdi pia ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi Februari akiwashinda Fadlu Davids na Fred Felix Minziro. Ushindi huu umetokana na mafanikio makubwa ya Yanga SC katika mwezi huo, kwa matokeo mazuri mfululizo.

Dube Mchezaji Bora wa Februari Ligi Kuu NBC 2024/25
Dube Mchezaji Bora wa Februari Ligi Kuu NBC 2024/25

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), tuzo hizo hutolewa kwa kuzingatia viwango vya wachezaji na makocha wa mwezi husika, ambapo vigezo kama vile idadi ya mabao, pasi za mabao na mafanikio ya timu huzingatiwa.

Baada ya kuonyesha kiwango kizuri mwezi Februari, mashabiki wa Yanga SC watakuwa na matumaini kuwa Dube ataendeleza wimbi lake katika mechi zijazo, huku timu yake ikipambana kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

CHECK ALSO: