M-Bet Kusitisha Udhamini Wake na Simba

M-Bet Kusitisha Udhamini Wake na Simba | Katika hali inayotikisa ulimwengu wa soka nchini, kampuni ya kamari ya M-Bet imeomba kukatisha mkataba wake wa udhamini na Simba SC mwishoni mwa msimu wa 2024/2025.

M-Bet Kusitisha Udhamini Wake na Simba

Mkataba huo wenye thamani ya shilingi bilioni 26.1 ulitiwa saini rasmi Julai 14, 2022 na kuzinduliwa kwa hafla maalum Agosti 1 mwaka huo. Mkataba huo ulikuwa wa miaka mitano, lakini mwisho wa msimu huu, ni miaka mitatu tu itakuwa imepita.

Klabu ya Simba SC ambayo kwa sasa ni miongoni mwa klabu zenye mafanikio makubwa nchini Tanzania, imekubali ombi la M-Bet la kusitisha mkataba na tayari imeanza mchakato wa kutafuta mfadhili mpya wa kuendelea kuisaidia kifedha.

M-Bet Kusitisha Udhamini Wake na Simba
M-Bet Kusitisha Udhamini Wake na Simba

Sababu za M-Bet kusitisha udhamini huu hazijawekwa wazi, lakini hatua hiyo inaweza kuwa na athari kwa klabu, hasa kifedha. Hata hivyo, uongozi wa Simba SC umeonyesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha klabu hiyo inapata mfadhili mwingine mwenye hadhi ya juu ili kuendeleza mafanikio yake ndani na nje ya nchi.

Mashabiki wa klabu na wadau wa soka bado hawajajua mustakabali wa udhamini wa timu hiyo huku macho na masikio yao yakiwa yameelekezwa kwa uongozi wa Simba SC katika harakati zake za kutafuta mbadala wa M-Bet.

Je, Simba SC itapata mfadhili mpya mwenye hadhi ya juu?

Kwa kuwa Simba SC ni miongoni mwa klabu kubwa barani Afrika, kuna fursa kubwa ya kupata wadhamini wapya wenye uwezo mkubwa wa kifedha. Wafuasi wa klabu hiyo wanatumai usimamizi utashughulikia suala hili haraka ili kuhakikisha hali ya kifedha ya timu inabaki kuwa sawa.

CHECK ALSO: