Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu England Leo Machi 16, 2025

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu England Leo Machi 16, 2025 | London derby na Manchester United ugenini

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu England Leo Machi 16, 2025

Ligi kuu ya Uingereza inaendelea leo Machi 16, 2025 kwa mechi tatu kali zikiwemo mbili za London derby na Manchester United wakikabiliwa na mtihani mgumu ugenini dhidi ya Leicester City.

Ratiba Kamili ya Mechi za Leo:

📌 16:30 | Arsenal vs Chelsea 🏟️ Emirates Stadium
📌 16:30 | Fulham vs Tottenham 🏟️ Craven Cottage
📌 22:00 | Leicester City vs Man United 🏟️ King Power Stadium

Arsenal dhidi ya Chelsea – London derby

Arsenal watakuwa wenyeji wa Chelsea kwenye Uwanja wa Emirates kuanzia saa 4:30 asubuhi. Mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku Arsenal wakihitaji pointi tatu ili kuendeleza mapambano yao ya kuwania ubingwa, huku Chelsea wakisaka nafasi ya kumaliza katika nafasi nne za juu.

Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu England Leo Machi 16, 2025

Fulham dhidi ya Tottenham – Derby nyingine ya London

Wakati huo huo, Fulham watakuwa wenyeji wa Tottenham Hotspur katika uwanja wa Craven Cottage. Spurs wanapigania kuimarisha nafasi yao kileleni, huku Fulham wakihitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi yao kwenye ligi.

Leicester City vs Manchester United – Van Nistelrooy dhidi ya waajiri wake wa zamani

Katika mechi ya mwisho ya wiki itakayoanza saa 10:00 Jioni, meneja mpya wa Leicester City, Ruud Van Nistelrooy atakuwa na kibarua kigumu dhidi ya klabu yake ya zamani, Manchester United, kwenye Uwanja wa King Power. United wanahitaji ushindi ili kuweka hai matumaini yao ya Ligi ya Mabingwa, huku Leicester wakipambana kukwepa kushuka daraja.

CHECK ALSO: