Uwanja Mpya AIRTEL STADIUM Kuzinduliwa Machi 24 | Singida Black Stars Kuzindua Uwanja Mpya ‘AIRTEL STADIUM’.
Klabu ya Singida Black Stars imepiga hatua muhimu katika maendeleo ya soka kwa kutangaza uzinduzi wa uwanja wake mpya wa AIRTEL STADIUM Machi 24, 2025. Uwanja huu utazinduliwa kwa mechi ya kirafiki kati ya Singida Black Stars na mabingwa wa kihistoria, Yanga SC.
Uwanja Mpya AIRTEL STADIUM Kuzinduliwa Machi 24
Katika taarifa rasmi ya klabu, Singida Black Stars imethibitisha kuwa uwanja huo umejengwa kwa viwango vya kimataifa na unatarajiwa kuwa uwanja mkubwa wa mashindano ya kitaifa na kimataifa. Hii ni hatua muhimu kwa klabu hiyo inayoendelea kuwekeza katika miundombinu yake ili kukuza soka la Tanzania.
Je, hili ni somo kwa Simba na Yanga?
Kwa muda mrefu, klabu kubwa za Tanzania, Simba SC na Yanga SC, zimekuwa zikitegemea viwanja vinavyomilikiwa na serikali mfano Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi zao za nyumbani. Licha ya mafanikio yao makubwa ndani na nje ya nchi, bado hawajaweza kuulinda uwanja wao wenyewe.

Uwekezaji wa Singida Black Stars katika UWANJA wa AIRTEL unaweza kuwa fundisho kwa klabu kubwa kama Simba na Yanga kuelewa umuhimu wa kuwa na viwanja vyao. Kuwa na uwanja wa kisasa kunazipa klabu uhuru wa kupanga ratiba za mechi, kuongeza mapato kupitia matukio mbalimbali, kuboresha mazingira ya mazoezi na maandalizi ya timu/Uwanja Mpya AIRTEL STADIUM Kuzinduliwa Machi 24.
Manufaa ya vilabu kuwa na uwanja wao wenyewe:
✅ Uhuru wa kupanga mechi bila kutegemea viwanja vya serikali
✅ Ongeza mapato ya klabu kupitia mauzo ya tikiti, utangazaji na mikataba ya kibiashara
✅ Weka mazingira bora kwa wachezaji kufanyia mazoezi na kujiandaa na mechi
✅ Kuongeza thamani ya klabu na kuifanya kuvutia wawekezaji zaidi
Kufunguliwa kwa AIRTEL STADIUM ni hatua muhimu kwa Singida Black Stars na soka la Tanzania kwa ujumla. Wakati klabu kama Azam FC tayari ina uwanja wake (Azam Complex), ni wakati sasa kwa Simba SC na Yanga SC kuanza mchakato wa kujenga viwanja vyao ili kuimarisha miundombinu na mustakabali wa muda mrefu wa klabu zao.
CHECK ALSO:
Weka maoni yako